Press Launch Searching For Peace

PRESS CONFERENCE : SEARCHING FOR A COMMON GROUND FOR PEACE IN ZANZIBAR HELD ON 26th NOVEMBER 2019. PROJECT FUNDED BY EUROPEAN UNION.

Mradi umeandaa majukwaa ya vijana, wanawake, viongozi wa dini na
mahusiano ya maafisa wa serikali kwa njia ya mazungumzo na mashirikiano kuhamasisha shughuli za kitamaduni na michezo ambazo huwaunganisha watu katika jamii.

Mradi huu wa kutafuta Amani (Searching for a Common Ground for Peace)
utatekelezwa Unguja na Pemba. Utakuwa wa kipindi cha miezi 12 kuanzia mwezi Oktoba 2019 hadi Septemba 2020. Tunaitazama miezi hii 12 kama
hatua ya kujifunza. Baada ya tathmini mradi utabainisha malengo na shughuli za kuendeleza katika miezi 12 ijayo ya kabla, wakati na baada ya
uchaguzi wa 2020.

Njia moja ya kufanikisha mabadiliko ni kukuza mshikamano miongoni mwa watu wa dini na siasa ili kuwafahamisha na kuwazindua wadau wote wa amani hapa Zanzibar.

Mradi huu ni fursa na wito kwa Serikali yetu tukufu ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini, viongozi wa siasa na wafuasi wao pamoja na jamii nzima ikubali na kushiriki katika mradi huu na kuwa msaada
kwa ustawi wa nchi ya Zanzibar. Mradi utakuza uelewa wetu kuhusu amani, utafufua na kuchochea ushirikiano wa viongozi wa kisiasa na kidini. Tunatarajia mazingira wezeshi na jamii nzima itahamasishwa kujitolea kwa ajili ya kujenga umoja na amani. Amani inaweza kupatikana tu pakiwapo maelewano yanayoweza kufikiwa kwa njia ya mazungumzo ya hiari. Kuongeza maelewano na mashirikiano ya kidini na kitamaduni miongoni mwa jamii kwa kuanzisha mazungumzo ya pamoja kwa ujenzi wa amani Zanzibar.

PRESS CONFERENCE : SEARCHING FOR A COMMON GROUND FOR PEACE
PRESS CONFERENCE : SEARCHING FOR A COMMON GROUND FOR PEACE